![]() |
Bi Moza akiwa akimshindikiza
mtoto wake Moh'd Saidi,
Nchini India kwa matibabu
|
Bi Moza Moh'd Khamis anapenda tena kutoa shukurani za dhati kwa wale wote waliochangia kwa hali na mali kwa mtoto wake Moh'd Said Moh'd, kwenda kufanyiwa matibabu ya upandikizaji wa figo, nchini India.
Mapema asubuhi ya leo Bi Moza aliongea na blog ya swahilivilla ili kutoa taarifa kwa kukamilika safari yake ya kwenda nchini India pamoja na kutaka tumuombe Dua za kumtakia kila la kheri katika safari hiyo.
Moh'd Said Moh'd ameondoka leo Jumanne Juni 9, katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuelekea Nchini India kwaajili ya matibabu yake.
Napenda kuchukua fursa hii kwa niaba ya Tanzania Bloggers Network (DMV) na waTanzania wote waishio Nchini Marekani, kumtakia kila la kheri Ndugu yetu Moh'd Said Moh'd katika matibabu yake huko Nchini India.
Napenda kuchukua fursa hii kwa niaba ya Tanzania Bloggers Network (DMV) na waTanzania wote waishio Nchini Marekani, kumtakia kila la kheri Ndugu yetu Moh'd Said Moh'd katika matibabu yake huko Nchini India.
M/Mungu amjaalie wepesi katika safari yake na ampe afuweni na mafanikio katika mipangilio yote matibabu yake. Ameen.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...