
Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (katikati) wakiwasili kwenye ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo kabla ya ziara ya kuelekea katika kijiji cha Chasimba kukagua miradi inayofadhiliwa na TASAF katika wilaya ya Bagamoyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Ladislaus Mwamanga.(Picha na Zainul Mzige).
Na Modewjiblog team, Bagamoyo
SERIKALI ya Hispania imetoa shilingi bilioni 3.1 kusaidia miradi ya maendeleo ya jamii nchini ambayo mingine inatekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii, TASAF.
Fedha hizo zimetolewa kupitia mfuko wa maendeleo endelevu (SDGF) zilizotolewa kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanya shughuli zake hapa nchini.
Mashirika hayo ni Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ,Shirika la Umoja wa Mataifa la watoto (UNICEF) , Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu (UNFPA), na Shirika la Kazi Duniani( ILO).
Hayo yamesemwa katika ziara ya Balozi wa Hispania nchini, Luis Cuesta Civis na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez katika kijiji cha Chasimba kilichopo wilayani Bagamoyo, Pwani jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...