Mbunge wa Jimbo la Sengerema na aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja amekanusha taarifa za kukutwa na tuhuma za ufisadi uliopelekea kuvuliwa uwaziri.
Akizungumza wakati wa kutangaza rasmi nia ya kuwania urais, Ngeleja  
amesema wananchi wengi wamekuwa wakidhani kuwa aliondolewa katika wadhifa huo kwa kutumia madaraka vibaya jambo ambalo si sahihi. 

Ameongeza utaratibu uliofanyika kumuondoa ni utaratibu wa kawaida na kuwa unaweza kutumika hata bila ya kuwa na udhaifu katika uongozi.

Ameongeza kumekuwa na baadhi ya baadhi ya watu wanaoeneza habari hizo kwa leo la kumchafua.
Willim Ngeleja anaungana na viongozi wengine wa siasa kutangaza nia ya kugombea urais. BOFYA VIDEO JUU KUMSIKILIZA. Hebu tujiulize. Kwa nini Takwimu za uchumi nchini zinaonyesha Uchumi ukikuwa kwa wastani wa asilimia 7% takribani kwa muongo mzima wa takribani miaka 10 mfululizo lakini umasikini umekuwa ukipungua kwa asilimia 2% tu? BOFYA VIDEO JUU KUSIKILIZA

Ingawa nafasi ya Urais imeombwa na wanachama wengi, Ngeleja atoa fursa kwa watanzania kumtathimini, na si kwa maneno ya mtaani bali kwa takwimu za utendaji kazi ikiwa ni sambamba na kuifuatilia ripoti ya CAG na ESCROW kuisoma kurasa hadi kurasa.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2015

    Matatizo ya wananchi hayajibiwi kwa hotuba, yanajibiwa kwa vitendo!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2015

    Nategemea vijana zaidi watatangaza nia hata kupitia vyama vya upinzani kumbuka Nyerere alianza kutawala na miaka 35.. Nimemwona yule wa Mzumbe pengine wengine watajitokeza baadaye. Hata kama usipoenda mbali itakujengea CV.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...