Mkurugenzi Mtendaji wa HUAWEI Tanzania Peter Zhang,
akizungumza na waandishi wa habari juu ya uwekezaji katika
Tekinolojia ya ICT nchini.Mazungumzo hayo yalifanyika Makao makuu
ya HUAWEI Tanzania jijini Dar es Salaam.
Tarehe 18 na 19 Juni 2015, ndani ya ukumbi wa Julius Nyerere International
Convention Centre (JNICC) uliopo mkoani Dar es Salaam, kampuni ya Huawei
Tanzania itashirikiana na Wizara ya mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kufanya
kongamano la sekta ya Teknolojia ya IT. Kongamano hili litazungumzia teknolojia
mpya ya IT ikiipa kipaumbele sekta mpya ya kuhifadhi data kwa kutumia njia ya
mawingu/cloud storage.
Lengo na dhumuni ya kongamano hili ni kuendelea kuwawezesha Watanzania
kwa njia moja au nyingine kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
kila mmoja wetu anaelewa kua kwenye karne hii ya mawasiliano; teknolojia ya
habari na mawasiliano ni muhimu sana hususani katika shughuli zetu za kila siku
ziwe za kibinafsi au za kibiashara .
Kwa kupitia teknolojia ya Habati na Mawasiliano, dunia inakua connected zaid na
zaid huku viwanda vilivyopo vikihitaji revamp kuhakikisha biashara inaendeshwa
efficiently and sustainability.
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano imewezesha kwa kiasi kikubwa ukuaji wa
sekta mbalimbali na kufanya ongezeko la uvumbuzi wa vitu mbalimbali na hivyo
kupelekea kuongezeka kwa mahitaji ya employment hususani kwa upande wa
vijana
Huawei Technologies Tanzania co. Ltd, imekua katika kiini cha mzunguko wa
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ulimwenguni ; ikiendesha shughuli zake
katika kila nchi mbalimbali duniani. Huawei imejizatiti huku kuhakikisha kua
kiongozi kwenye uvumbuzi wa teknolojia mpya pamoja na ukuaji na ongezeko la
maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya kilimo, viwanda, biashara,
...... n.k
Kampuni ya Huawei Tanzania imewekeza nchini Tanzania kwa kiasi kikubwa na
has commited zaidi kwenye ukuaji wa maendeleo ya sekta ya Habari na
Mawasiliano nchini. Katika sekta hii ya Habari na Mawasiliano, kampuni ya
Huawei Tanzania imelenga Zaidi kwenye upande wa elimu na mawasiliano na
imeahidi kuendelea kufanya hivo.
Mwaka 1998, Kampuni ya Huawei Tanzania ilianza shughuli zake nchini
Tanzania na mpaka hadi leo ina wafanyakazi Zaidi ya 315 kupelekea kufanya
idadi ya watanzania kua na Zaidi ya asilimia 75. Toka ianze shughuli zake za
kukuza Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hapa nchini, Kampuni ya Huawei
Tanzania imekua ikishikiriana na wadau wengine mbalimbali wa ICT ikiwemo
mashirika binafsi, mashirika ya uma pamoja na Serikali ya Tanzania.
Kampuni ya Huawei Tanzania inaongoza katika sekta ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano nchini Tanzania na imekua ikishirikiana na wadau wengine wa
mawasiliano kama Tigo, Vodacom, Airtel, Zantel na TTCL katika kuchangia
ukuaji wa individuals kwenye hii sekta (ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...