Jambo Bukoba ni Shirika lisilokuwa la Serikali linalofanya kazi mkoani Kagera kwa kushirikiana na serikali ya Mkoa.
Mwanzilishi wa Jambo Bukoba ni Bw. Clemence Mlokozi ambaye asili yake ni Mkoani Kagera katika Wilaya ya Missenyi Kijiji Ishozi na anaishi nchini Ujerumani.
Jambo Bukoba ilianzishwa Mkoani Kagera kwa kusaidia watoto hasa wanafunzi wa shule za msingi kuanzia miaka 5 hadi 19 kujenga afya zao kimichezo ili kujikinga na Maabukizi ya UKIMWI, kuweka haki sawa katika elimu kupitia michezo kwa wasichana na wavulana.
Shirika hili chini ya mwanzilishi wake Bw. Mulokozi tangu kuanzishwa kwake mkoani Kagera limekuwa likiwafunza watoto katika shule za msingi kila wilaya michezo midogo midogo ya kujenga ushirikiano wa pamoja hasa watoto wa kike kujiamini
na kushirikiana zaidi na wenzao wa kiume.
Kongamano hilo litafanyika katika Mji wa Berlin, Germany kuanzia tarehe 27 juni - 06 julai, 2015 na wawakilishi hao watakaa huko juma moja/ siku saba. Msafara huo Unaongozwa na Gonzaga Stephen ambaye ni Meneja wa Mradi huo wa Jambo Bukoba akisaidiana na msaidizi wake Bi. Imani Paul. Pia watandamana na Walimu mmoja mmoja kwa kila Shule za Msingi baadhi kutoka Kila Wilaya saba.
Walimu hao ni Peace Saleand kutoka Biharamulo- Rubondo Shule ya Msingi. Grace Wamara kutoka Shule ya Msingi Tumaini ambayo Ipo Bukoba Mjini. Alistidia Bijura kutoka Shule ya msingi Kaisho - Kyerwa.
Elizabeth John kutoka Rulenge Shule msingi - Ngara
Abela Ndeyokobora Kutoka Shule ya Msingi Kayanga - Karagwe
Jeni Mulokozi Kutoka kashekya Shule ya Msingi - Misenyi
William Magosa kutoka Karalo Shule ya Msingi -Karagwe
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...