Na Mwashungi Tahir na 
Rahma Khamis-Maelezo Zanzibar 
Chama cha Mapinduzi CCM kimelaani kitendo kilichofanywa na Wajumbe wa Baraza la wawakilishi kupitia chama cha Wananchi (CUF) kutoka ndani ya kikao halali cha Baraza la Wawakilishi wakati wa mjadala wa kupitisha Mswaada wa sheria wa matumizi ya fedha za serikali kwa mwaka 2015/2016 ukiwa bado unaendelea. 
 Akizungumza na Waandishi wa habari Ofisini kwake Kisiwandui Naibu Katibu mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai amesema kitendo kilichofanywa na Wawakilishi hao hakikuwafurahisha kwani kinaashiria uvunjifu wa amani ulipo nchini.
 Amefahamisha kuwa katika hali hiyo isiyo ya kawaida Wajumbe kutoka CUF waliamua kutoka nje ya Baraza baada ya Juma Duni Haji kuwasilisha hoja binafsi iliyodai “CUF hairidhishwi na Zoezi la uandikishaji la daftari la kudumu la wapiga kura linaloendeshwa Wilaya ya Magharibi kwa kugubikwa na udanganyifu wa kuandikisha watu wasio na sifa. 
 Hata hivyo Vuai amedai kuwa Madai ya CUF hayana msingi wowote na kwamba Lengo lao ni kuwazuia watu Unguja wasipate fursa ya kuandikishwa ipasavyo kwenye Daftari hilo ili kujiandalia mazingira ya Ushindi. 
 Aidha Vuai ametoa wito kwa WanaCCM kujitokeza kwa wingi katika Vituo vya Uandikishaji ili waweze kutimiza haki yao ya kidemokrasia. Ameviomba Vyombo vuya Dola viweke ulinzi wa kutosha ili wananchi wote wapate haki yao ya kuandikishwa katika Daftari bila wasiwasi wowote. 
 Vuai amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kuweza kusimamia Maendeleo ya haraka ya Zanzibar jambo ambalo limewezesha ukuaji wa uchumi na huduma mbali mbali za kijamii. 
 Amesema mafanikio mengine ya kupongezwa Dkt Shein ni pamoja na kusimamia Amani na utulivu katika Visiwa vya Unguja na Pemba jambo ambalo limewezesha wazanzibar wote kushiriki katika shughuli zao za kisiasa,kiuchumi na kijamii.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akizungumza na Waandishi wa Habari katika Afisi kuu CCM Kisiwandui ambapo amelaani hatua ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Chama cha CUF kugomea Vikao vinavyoendelea vya Baraza la Wawakilishi hapo Jana.Picha na Miza Othman-Maelezo Zanzibar
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakichukuwa maeelezo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari katika Afisi kuu CCM Kisiwandui. Vuali amelaani hatua ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Chama cha CUF kugomea Vikao vinavyoendelea vya Baraza la Wawakilishi hapo Jana. picha na Miza Othman-Maelezo Zanzibar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...