Na Avila
Kakingo,Globu ya Jamii.
JENGO la
ghorofa 16 lililopo mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es Salaam linatarajiwa
kubomolewa kwa kuwa linadaiwa kujengwa chini ya kiwango.
Amri hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki
wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,amesema kuwa uwepo wa
jengo hilo ambalo limejengwa chini ya kiwango limezua hofu kubwa kwa wakazi wa
eneo hilo,kwani jengo hilo lipo karibu na jengo lingine lililokuwa na ghorofa
16 ambalo lilianguka wakati wa ujenzi wa ghorofa hilo ukiendelea.
Hatua za ubomoaji
wa jengo hilo zinaendelea wakati wakazi wa eneo hilo wameombwa kuepuka na madhara yatakayojitokeza
katika ubomoaji wa jengo hilo.
Kampuni
ambayo imepewa dhamana ya ubomoaji wa Jengo hilo ni kampuni ya Kichina ya ERJE ambayo wanasubiri itekeleze
wajibu wake katika kubomoa jengo hilo.
Jengo la Ghorofa 16 ambalo linatakiwa kubomolewa lililopo katika mtaa wa Indira Ghadhi jijini Dar es Salaam.(Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.)
Linabomolewa kwa sababu ya wasiwasi tu wa wakazi wa eneo hilo au wataalamu wamepima na kuona kuwa liko chini ya kiwango?!
ReplyDelete