Jarida la Wizara ya Maliasili Makumbusho na Utalii katika mji wa Trollhättan na Vänersborg limeijumuisha Tanzanian Restaurant - Lunch by chef Issa kwenye orodha ya migahawa bora katika miji hiyo miwili ni jambo la kujivunia hasa mafanikio haya ndani ya miezi miwili tangu kufunguliwa
IMG-20150616-WA0008
Jarida la makala ya biashara na uwekezaji la Fokus Väst la mji wa Trollhättan Sweden limethibitisha rasmi nakujivunia Tanzanian Restaurant - Lunch by chef Issa kua ni mgahawa halisi wa kiafrika mkubwa kuliko yote kwa bara la ulaya. Kusoma taarifa hiyo bofya link ya Fokus magazine http://en.calameo.com/read/0028316377167713a84d5 Habari ipo ukurasa wa mwisho
IMG-20150616-WA0013 IMG-20150616-WA0011 IMG-20150616-WA0009
Karibu na Like Facebook page ya Tanzanian restaurant - Lunch by Chef Issa https://m.facebook.com/profile.php?id=829878737101969 na kuwasiliana naye moja kwa moja kupitia ukarasa huo.
IMGL23721
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mtaalamu wa kimataifa wa mambo ya mapishi aishiye Sweden Chef Issa Kapande ambaye mwaka jana alikuwa katika timu ya taifa ya Sweden kwenye mashindano ya kombe la dunia la mapishi walikoibuka na medali ya dhahabu hivi karibuni alipokuwa nchini Sweden ziara ya kikazi na kukutana na Watanzania waishio nchini humo. Chef Issa, ambaye hivi karibuni amefungua mgahawa mkubwa kuliko yote wa Ki Afrika katika Ulaya yote mjini Trolhattan, nje kidogo ya jiji la Stockholm, wenye uwezo wa kuchukua watu 400 kwa wakati mmoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 23, 2015

    Nikukupongeza to Chef Issa endeleza kazi nzuri, lakini na sisi usisahau kutuandikia vitabu vya mapishi ikiwezekana kwa kiswahili tunatarajia utalii utaongezeka tutahitaji kuongeza ujuzi wa kupiga vyakula mbalimbali hapa nchini.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 23, 2015

    Mmeuona huo uzalendo wa kitanzania katika sare ya Chef.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...