Afisa Habari za Utalii Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon (kushoto) akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali za utalii na vivutio vyake nchini Tanzania kwa baadhi ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali vikiwemo vya utalii nchini Zimbabwe waliofika katika banda la Tanzania kwenye maonyesho ya nane ya Kimataifa ya Utalii Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) kupata taarifa mbalimbali za vivutio vya utalii wa Tanzania yaliyomalizika jana jijini Harare katika ukumbi wa hoteli ya Rainbow Towers.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)
Afisa Habari za Utalii Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon (kulia) akibadilishana mawazo na wananfunzi wa Belvedere Technical Teachers College nchini Zimbabwe, Francisca Chipuriro (kushoto) na Natalie Takavarasha (katikati) wakati walipotembelea banda la Tanzania kwa ajili ya kupata taarifa mbalimbali za utalii wa Tanzania na vivutio vyake siku ya ufunguzi rasmi wa maonyesho hayo yaliyomalizika juzi jijini Harare katika hoteli ya Rainbow Towers.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...