Na Sultani Kipingo 
wa Globu ya Jamii
Karibu kila mtu duniani leo hii analijua neno “Selfie” ambalo maana yake ni picha ya mnato ya kujipiga mwenyewe kwa kujielekeza Camera, lakini ni wachache wanaojua kwamba neno hilo lilianza kuvuma muda wa mwaka juzi tu, pale watunzi wa kamusi za Oxford walipoliweka kwenye kamusi zao na kulitaja kuwa ndilo neno la mwaka 2013 na kulipa maana hiyo ya kujipiga picha mwenyewe na kutundikwa kwenye mitando ya kijamii.

Ingawa matumizi ya neno “Selfie” linaonekana ni la kileo, lakini tendo la mtu kujipiga picha mwenyewe si  geni kabisa kwani tangia miaka ya awali ya sayansi ya picha za mnato aghalabu watafiti na waendelezaji wa sayansi hii walizoea kujipiga picha wenyewe katika kufanikisha tafiti zao. 
Hapo elewa kwamba sayansi hii ilianza tokea miaka ya 1800 mwanzoni na katikati ya miaka hiyo na kuendelea

Hiyo hapo juu ndiyo “Selfie” inayoaminika kuwa ni ya kwanza kabisa kupigwa duniani na kuwepo katika kumbukumbu iliyopigwa mwaka 1839 na mkemia na mtafiti wa picha za mnato aitwaye Robert Cornelius wa jiji la Philadelphia nchini Marekani (BOFYA HAPA) .

 Akitumia mbinu zilizotumia wakati huo, huyu bwana alijipiga picha hii kwa kufunua lensi (zamani hakukuwa na kitufe cha kubofyea, ilikuwa unafunua lensi kwa muda maalumu na kisha kuiziba) na akaenda mbele ya Camera ambako alikaa kwa muda unaotakiwa lensi kuwa wazi, kisha akarudi na kuiziba. Nyuma ya hii picha akaandika  “The first light Picture ever taken. 1839.”  Yaani “Picha ya mwanga ya kwanza kabisa kuchukuliwa. 1839”

Globu ya jamii imefanya utafiti huu wa kubaini picha moja ya mnato ya watu wanne wanaojipiga "Selfie" mwaka 1920  (kulia) inayozunguka kwenye mitandao ya kijamii   na kudaiwa kuwa ndiyo “Selfie”  ya  awali kabisa (BOFYA HAPA). Hivyo ukweli ndio huo hapo juu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 22, 2015

    MR.Bean naye alikuwa mkali wa "selfie"

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 22, 2015

    Inaonekana selfie za zamani zilikuwa zinapigwa kwa kutumia kamera kubwa zaidi, za black and white.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...