Baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya sambamba na wadau katika tasnia hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bi. Rose Malo na Adam Anthony mwakilishi toka OSIEA (walioketi) mara baada ya warsha fupi kwa wasanii hao juu ya umuhimu wa Sanaa ya muziki katika kuhamasisha Wananchi kujiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura, kupitia Kampeni yake ya #KuraDili2015. Kampeni hiyo itawawezesha wasanii hao kutunga Wimbo Maalum wa kuhamasisha watu kujiandikisha hasa vijana waliofikia umri wa kupiga kura. Warsha hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Mgahawa wa ....., Upanga jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mratibu wa Warsha hiyo kutoka Kampuni ya Masoko, Costantine Magavila.
Mratibu wa Warsha hiyo kutoka Kampuni ya Masoko, Costantine Magavila akifafanya jambo kwa Wasanii wa Muziki wa kizazi kipya juu ya umuhimu wao katika kuhamasisha vijana kujiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura, kupitia Kampeni yake ya #KuraDili2015.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Stamina akieleza jambo kwa wasanii wenzake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...