Kampenii dhidi ya ugonjwa wa usonji yazinduliwa • 
Familia nyingi Tanzania hazina ufahamu wa hali hii
Kliniki ya Lotus kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, zimeanzisha kampeni mpya inayolenga kuelimisha uma kuhusu ugonjwa wa usonji (autism), ambao watanzania wengi hawaufahamu.Ugomjwa huu sasa unatishia familia nyingi kwani dalili zake huanza utotoni na zinaweza kuendelea hadi ukubwani.
Akizugumza wakati wa uzinduzi huo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha Kuhudumia watu wenye Usonji Tanzania, Dk. Stella Rwezaula ambaye pia ni mtaalamu wa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na pia ana mtoto mwenye ugonjwa huo, aliishukuru Kliniki ya Lotus kwakuwa katika mstari wa mbele kuanzisha kampeni hiyo ili kuwaelimisha watanzania kuhusu ugonjwa huo.
“Ni vyema ugonjwa huu ukigundulika mapema na kutibiwa ili aliyeathirika aweze kupona na kuishi maisha ya kawaida hapo baadaye kulingana na athari aliyoipata. Mtoto kuanzia miaka 0-6 anawezakutibiwa vizuri na kusaidia kubadilisha maisha yake,” alisema.
Alisema watoto wenye hali hii wana shida katika kuwasiliana na tabia zao ni kurudia rudia mambo anayofanya mara kwa mara na pia watuwengi wenye ugonjwa huu wananamna yao ya kujifunza, kusikiliza na kuitika.
“Mfano wa hali hii ni kwamba katikahali ya kawaida, mtoto wa mwaka mmoja hutabasamu au kuwa na furaha kila wakati, huiga mambo mbalimbali anayoona na kufuatilia vitu anavyoviona vikisogea, lakini mtoto mwenye ugonjwa huu hafanyi vitu hivi,”alisema.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kliniki ya Lotus, Dialla Kassam alisemamuelewa bado ni mdogo nchini Tanzania na watoto wengi huathiriwa na kuja kujukilana wakati hali imeshakuwa mbaya zaidi.
“Kukosa uelewa wa hali hii ya watoto wenye mahitaji huwafanya walimu na wazazi kudhani watoto ni watundu, wavivu au wanakera na wakati mwingine huadhibiwa kwa sababu hiyo wakati kwamba watoto hawa wanahitaji uangalizi wa karibu, kupendwa na kupata msaada kutoka kwa
walimu na wenzao,” alisema.
Alisisitiza umuhimu wa kuwafundisha walimu na wazazi kuhusu watoto hawa wenye mahitaji maalumu ili waweze kuwasaidia kuishi na kukubalika katika jamii.Alisema kliniki yake inahudumia watoto wenye mahitaji ya aina hii jijini Dar es Salaam na kuwa timu yake ina wataalamu mbalimbali wanaofanya kazi pamoja ili kutoa elimu kuhusu watoto wenye matatizo haya.
“Hii inafanyika kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa kwa kutoa elimu kwa wadau mbalimbali wakiwemo walimu na wazazi kupitia warsha,mafunzo mbalimbali, kutafuta wafanyakazi wa kujitolea na kutoa rasilimali kwa taasisi mbalimbali kama Shule ya Mbuyuni ya watu wenye ugonjwa huu,” alisema. 
Alisema kliniki mbalimbali kuhusu ugonjwa huo hufanyika katika Hospitall ya Taifa ya Muhimbili kila Alhamisi na kwamba Chama Cha Watu Wenye Usonji-Tanzania (NAPA-T) kimekuwa kikisaidia.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Lotus Clinic, Dialla Kassam (katikati), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum ya kueneza uelewa kuhusu tatizo la usonji ‘Autism’ nchini Tanzania iliyondaliwa na Lotus Medical Clinic kwa
kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na taasisi ya Autism Education Trust ya Uingereza. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Kuhudumia watu wenye Usonji Tanzania, Dk. Stella Rwezaula na Daktari wa kufundisha kuongea, Nazreem Sumar.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Lotus Clinic, Dialla Kassam (katikati), akitoa utambulisho kwa meza kuu mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana katika uzinduzi huo. Kushoto ni Mtaalam wa Afya kutoka taasisi ya Autism Education Trust ya Uingereza, Kevin Baskerville, Mwenyekiti wa Chama cha Kuhudumia watu wenye Usonji Tanzania, Dk. Stella Rwezaula (wa pili kushoto), Daktari wa kufundisha kuongea wa Lotus, Nazreem Sumar (wa pili kulia) na Daktari Fathema Hasham.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 01, 2015

    Hongereni sana, usonji ni tatizo linalozidi kukua na jamii haina uelewa mkubwa. Clinic ya Lotus iko wapi? na shule ya mbuyuni nayo iko wapi?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 01, 2015

    Fanyeni uchunguzi vizuri, usonji (autism) yawezekana sio ugonjwa bali mabadiliko chanya ya binadamu katika mageuko (evolution) yanayoendelea. La sivyo tutaingia kwenye mkumbo ambao huko Ulaya wameuingia kukwamisha makuzi ya mwanadamu.

    Na tatizo kubwa ni kwamba tunataka kila mtu awe kama watu wengine. Ukimkuta anayependa kuwa peke yake, hataki kuongeaongea, tayari unamchukulia kuwa mgonjwa, kumbe yeye ana uwezo wa kukuelewa kabla hata hujaongea kitu! Na sasa hivi tunawafungia Milembe watu ambao tungeelewa wasingestahili kuwa kule, labda wangefungiwa sehemu za ugunduzi wa mambo ya ajabu kutukwamua kwenye haya matatizo tuliyonayo. Wengine wanaweza wasione kama tuna matatizo makubwa, lakini hii tu kuunguza mafuta kwa ajili ya nishati ni balaa kubwa mno la Dunia hii kwa sasa!!

    Tuko kwenye kipindi kikubwa sana na muhimu cha mabadiliko, msishangae watoto wanazaliwa wanajua lugha fulani, au mahesabu, au wanakumbuka walikotoka kabla ya kuingia kwenye miili hii ya sasa, nk.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 01, 2015

    Kumbe autism ni usonji ni vizuri kufahamu hili

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...