Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akitia saini kwenye kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo ya Marehemu Jaji Mstaafu Samuel Luangisa nyumbani kwake kwa marehemu Kitendagulo,mjini Bukoba mkoani Kagera.Marehemu Luangisa ni miongoni  mwa Waasisi wa Taifa na katika vipindi tofauti tofauti alikuwa mkuu wa Mkoa wa Ziwa Magharibi (Kagera),Mbunge na Meya wa Manispaa ya Bukoba pamoja na nyadhifa nyingine.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Jaji Mstaafu Samuel Luangisa mapema leo asubuhi nyumbani kwake kwa Kitendagulo,mjini Bukoba mkoani Kagera.
Katibu Mkuu Ndugu Kinana na baadhi ya maofisa wa chama na ndugu na jamaa wa marehemu wakishiriki sala ya pamoja na kumuombea marehemu Mzee Samuel Luangisa nyumbani kwake Kitendagulo,mjini Bukoba mkoani Kagera
Katibu Mkuu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitia saini kwenye kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo ya Marehemu Mh. Samuel Luangisa nyumbani kwake mapema leo asubuhi,Kitendagulo,mjini Bukoba mkoani Kagera.

PICHA NA MICHUZI JR-BUKOBA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2015

    Sahihisho, Marehemu hajawahi kuwa jaji wala mwansheria.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2015

    Watu wanatoa heshima za mwisho wakiwa na kofia zao kichwani? Wanajeshi/Polisi/viongozi wa dini wanaruhusiwa kama sehemu ya mavazi yao.Kwa heshima unatoa kofia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...