Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara ya miezi 26 katika mikoa 31 nchini, ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. 

Mkutano huo umefanyika kwenye viwanja vya Furahisha, Kirumba jijini Mwanza jana jioni. Ndugu Kinana ambaye katika ziara hiyo ameambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, tayari wamesafiri umbali wa Km 193,537, kwa kufika katika Wilaya 163, majimbo 239, nusu ya vijiji na kata 1938 za Tanzania. Pia msafara wake ulitumia jumla ya saa 84 kuzunguka mikoa yote hiyo, na kusafiri kwa mitumbwi katika visiwa 16. Amehutubia jumla ya mikutano ya ndani/hadhara 1918 na kujikusanyia wanachama wapya 284300 ambapo kutoka upinzani 38984.
Aliyekuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya Chadema, katika uchaguzi mkuu uliopita, Twalib Ngika, akikabidhi Kadi ya Chadema kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana  baada ya kutangaza kuhamia CCM, wakati wa mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu huyo uliofanyika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza jana.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza jana jioni, ambapo amewataka viongozi wa chama na Serikali kutoka maofisini kwenda kwa wananchi kuzitafutia ufumbuzi kero zao.


Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akifafanua jambo mbele ya wakazi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake,alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara ya miezi 26 katika mikoa 31 nchini, ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. 

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiagana na wananchi mara baada ya kumaliza kuwahutubia kwenye Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza jioni ya leo,Kinana aliwahutubia wananchi na kuahidi kuwa bunge lijalo kwa upande wa CCM, litakuwa na mabadiliko makubwa kwa kuwapa nguvu wabunge kuihoji serikali kuhusu utendaji wake.
Ndugu Kinana akiwapungia mkono wananchi alipokuwa wakiwasili kwenye Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza, ambapo aliwahutubia wananchi na kuahidi kuwa bunge lijalo kwa upande wa CCM, litakuwa na mabadiliko makubwa kwa kuwapa nguvu wabunge kuihoji serikali kuhusu utendaji wake.
Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria mkutano wa CCM kwenye Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza jana.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...