Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini.Prof Anna Tibaijuka pamoja na mkuu wa mkoa wa Kagera,John Mongella wakishiriki katika kazi ya utandazaji wa umeme wa REA katika shule ya sekondari ya Nyakatanga,jimbo la Muleba Kaskazini mkoani Kagera wakati wa ziara ya Kuimarisha uhai wa chama,kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010 pamoja kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi
Umeme wa REA umesambazwa kwa kasi katika jimbo la Muleba Kaskazini,kama uonekanvyo katika nyumba hii katika kijiji cha Nshamba,wilayani Muleba mkoani Kagera.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Kinana (haonekani pichani) akikagua na kupata maelezo
kuhusiana na maendeleo ya mradi wa maji katika kata ya Nshamba wilayani
Muleba mkoani Kagera.
katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza jambo na Diwani wa CHADEMA wa kata ya Mushabago,Respikius Feruz,baada ya kuhudhuria mkutano wa hadhara katika kijiji cha Rushwa,Diwani huyo alionekana kuvutiwa mno na maneno ya Ndugu Kinana na pia alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini,Mh.Charles Mwijage kwa kazi nzuri anayoifanya jimboni mwake.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi basikeli kwa ajili ya Makatibu wa CCM kata zilizopo jimbo la Muleba Kaskazini, baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara. Baiskeli hizo zimetolewa na Mbunge wa jimbo hilo Charles Mwijage (kulia).
Katibu Mkuu wa CCM akikabidhiwa na Mbunge wa Muleba Kaskazini Mh.Charles Mwijage generata, kwa ajili ya kina mama wanaofanya shughuli za kilimo cha umwagiliaji.
Vijana wanaofanya kazi katika mradi wa mabwawa ya kufugia samaki wa Ruhanga, katika Kijiji cha Izigo mkoani Kagera, wakiwa kazini leo .
Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage akimpa maelezo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuhusu mradi wa mabwawa ya ufugaji samaki ya wajasiliamali, alipokagua mradi huo.
Wananchi wa kijiji cha Izigo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo wa hadhara.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akisisitiza jambo alipokuwa akiwahubia wananchi wa kijiji cha Izigo,Wilayani Muleba katika mkutano wa hadhara.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahubia wananchi wa kijiji cha
Izigo,Wilayani Muleba katika mkutano wa hadhara.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kulia) wakati akimtambulisha kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana, Mhariri wa zamani wa Tanzania Daima Asbert Ngurumo, ambaye alifika kwenye mkutano wa Katibu Mkuu huyo wa CCM uliofanyika katika kijiji cha Izigo, wilayani Muleba.
PICHA NA MICHUZI JR-MULEBA
Mwenye nyumba ya udongo iliyowekewa luku aamasishe kuchoma matofali ili ajenge nyumba bora yenye usafi, muonekano mzuri, ya gharama nafuu. Kusambaza umeme kuende pamoja na kuimarisha makazi ya wenyeji.
ReplyDeleteVingozi wasaidie mama aliye kwenye nyumba ya picha ya pili ajengewe nyumba kidogo kama picha ya namba 3. Tunasema tuimarishe uchumi halafu watu wanaishi kwenye mazingira ambayo hawapigi rangi nyumba zao hawapigi ripu hakuna viti wala vitanda, sasa kazi za mafundi na maseremala zitaongezeka vipi kama watu wengi wameamua kuishi kama babu zetu walivyoishi. Ujumbe tuboreshe maisha ya kila mtanzania na vipato vyao.
ReplyDeleteREA wanajitahidi, hata huyu jamaa kawekewa luku.
ReplyDelete