Jumamosi ya 6 Juni 2015 inasemekana haikuwa nzuri katika kambi ya FFU -ughaibuni baada ya msimu wa joto kuanza nchini ujerumani, kikosi maalumu cha kuangalia wanyama kiliungana na Kamanda ras Makunja kumsaka Bundi wa mkuu huyo wa Ngoma Africa Band, Bundi maarufu kwa jina la udi udi alichomoka katika banda maalumu katika makao ya Ras Makunja marufu kama himaya ya Anunnaki Alien.

 Kutoroka kwa Bundi huyo kumesababishwa na mbwa wa kamanda aitwae Kopro Dogi Domobaya, mbwa huyo anashutumiwa kwa kuwa mzembe na kuupiga kikumbo mlango wa banda la Bundi na kumfanya bundi kutoroka, kamanda Ras Makunja aliwambia kikosi cha kuangalia wanyama kuwa "huyu mbwa si mlinzi mzuri siku hizi amekuwa na utoto sana ! mbwa huyu tangu ampewe zawadi ya mpira na watoto wa jirani yeye kazi yake ni kucheza na mpira mpaka kavunja banda la Bundi.

 Ras Makunja akilalamika na kudai kuwa huyu mbwa akiendelea na uzembe atamfuta kazi,Pia inasemekana midudu hiyo imetengewa eneo maalumu katika himaya ya FFU-ughaibuni, Bundi huyo baadaye alirudi mwenyewe baada ya kutoweka kwa masaa kadha.
Kamanda ras Makunja akiwa nje ya himaya yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 09, 2015

    huyo kolokoloni nambari 2 Kopro Dogi domo baya lazima atimuliwe kazi,inakuaje
    awe bize na kucheza mpira tu na kusahau kazi yake

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 09, 2015

    duh ! Noma huyo dog angesababisha nembo ya himaya ya Anunnaki kutoweka !

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 09, 2015

    Kamanda huyo mlinzi dog domo baya hana maana si mtumishi mwema mfukuze kazi

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 09, 2015

    Dr.Slaa umewasikia watoto wa mbwa hao ? wataanza kukubwakia sasa hivi

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 09, 2015

    Ukiweka mbali vituko vyake kamanda ras makunja ni mtunzi mwenye kipaji nyimbo zake nazikubali sana, mistari yake uwa inachoma moyo na mara nyingine kuleta raha

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 09, 2015

    Ukiweka mbali vituko vyake kamanda ras makunja ni mtunzi mwenye kipaji nyimbo zake nazikubali sana, mistari yake uwa inachoma moyo na mara nyingine kuleta raha

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 09, 2015

    kikamanda ketu cha ffu-ughaibuni kufanya nae kazi lazima uwe imara na mjeshi wa kisawa sawa

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 09, 2015

    WAKUU NAJUA BAADA YA PURUKUSHANI HIZI LAZIMA HASIRA ZENU MTARUSHA SONG JIPYA LA KUTINGISHA ANGA

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 10, 2015

    Kamanda mkuu wa ffu-ughaibuni inasemekana ukiachia uwanamuziki wake jamaa yupo fit kwa mbio kila siku kilomita 5 joging sio mchezo

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 10, 2015

    Kamanda ni mfano mwema nasikia jamaa atumii kilevi chochote,avuti sigara mwangalifu sana katika vyakula pia mara nyingi usafiri na maji ya kunywa kutoka makao makuu ya FFU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...