katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwa ameambatana Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (aliyebeba mtoto),wakiwasalimia wananchi wa kijiji cha Nyakanazi,wilayani Biharamulo mkoani Kagera
Wananchi wa kijiji cha Nyakanazi pamoja na wapenzi/washabiki wa chama cha CCM wakishangilia kwa ujio wa Katibu Mkuu wa CCM Taifa,Ndugu Kinana mkoani Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwasalimia Wananchi wa kijiji cha Nyakanazi pamoja na wapenzi/washabiki wa chama cha CCM waliofika kumsikiliza mapema leo asubuhi,mkoani humo.Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na baadhi ya maofisa wa chama hicho wako ziarani kanda ya ziwa kwa siku 28 za  Kukagua utelekezwaji wa Ilani ya chama cha CCM ya mwaka 2010 pamoja na kuimarisha chama na kusikiliza matatizo ya wananchi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa mapema leo katika uwanja wa shule ya msingi Nyakanazi,Wilayani Biharamulo  mkoani Kagera,ambapo pia aliwasalimia wananchi wa kijiji hicho tayari kwa kuanza ziara rasmi mkoni humo. Kinana yupo Mkoani humu kwa ziara ya kikazi ya siku kumi ya Kukagua utelekezwaji wa Ilani ya Chama cha CCM ya mwaka 2010 pamoja na kuimarisha chama na kusikiliza matatizo ya wananchi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na wafuasi wa chama hicho wakikatiza kuelekea kwenye mkutano wa ndani na pia kuzungumza na kundi la Wafugaji
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na ujumbe wake akikatika kwenye moja ya soko katika kijiji cha Nyakanazi,Wilayani Buharamulo mkoani Kagera mapema leo asubuhi,akielekea kwenye mkutano wa kupokea taarifa za Chama na serikali pamoja na kuyasikiliza makundi ya Wafugaji kuhusiana na matatizo waliyonayo.

PICHA NA MICHUZI JR-KAGERA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2015

    ABDULAHMAN KINANA ANATAKIWA APEWE ZAWADI KWA KUFANYA KAZI VIZURI KULIKO KATIBU MWINGINE YEYOTE WA C.C.M

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...