Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitembelea shamba la ndizi na kahawa la mkulima wa Kahawa na Ndizi Ndugu Eustace Kubalienda Kishunji katika kijiji cha Mabila,wilayani Kyerwa mkoani Kagera
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa mkulima wa Kahawa na Ndizi Ndugu Eustace Kubalienda Kishunji ambaye ni mmiliki wa shamba la Ndizi,, Amesema shamba hilo lina miche 345 ambayo huvuna magunia 25 na ana shamba la migomba ambalo humpatia mavuno ya mikungu kwa mwezi 45.
Mzee Kishunji ambaye anaishi katika kijiji cha Kikukuru kata ya Mabira ameweza kusomesha watoto wawili katika vyuo vikuu vya Dar es salaam na Dodoma na amejenga nyumba ya kisasa yenye thamani kubwa ya fedha kutokana na kilimo bora cha kisasa.
Katibu
Mkuu Kinana yuko ziarani katika mikoa ya Kagera , Geita na Mwanza
akikagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010,
akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
Mkulima
bora wa migomba na kahawa katika Kijiji cha Mabira, Mzee Eustus
kishunju Ntibalienda (kulia) akimpatia maelezo Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana, kuhusu alivyoweza kufanikiwa katika kilimo cha mazao
hayo, Katibu Mkuu alipomtembelea mkulima huyo, akiwa katika ziara ya
kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama katika wilaya ya
Kyerwa, mkoani Kagera, leo.
Sehemu ya soko la biashara la kisasa na la kimataifa linalojengwa Kigorogoro,mpakani mwa Tanzania na Uganda.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (pichani kati) akiwa ameongozana na
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Mkuu wa mkoa wa
Kagera Mh.John Mongella wakijadiliana jambo mara baada ya kuzungumza na
wananchi wa Kijiji cha Kigorogoro, alipowasili katika kijiji hicho
kukagua ujenzi wa soko la kisasa na la Kimataifa katika kijiji hicho
leo.
Hhata
hivyo Kinana ameonesha kusikitishwa baada ya kujulishwa kuwa ujenzi wa
mradi huo, unaohitaji sh. bilioni 1.5 umesimama kutokana na serikali kuu
kukosa fedha.
Kutokana na hali hiyo, Katibu Mkuu wa CCM, amesema ni vema miradi
muhimu ya maendeleo iwekwe chini ya usimamizi wa halmashauri ya eneo
linalohusika badala ya serikali kuu.
Amesema, utaratibu wa kuifanya miradi ya aina hiyo kuwa chini ya
usimamizi wa serikali, umekuwa ukileta matokeo mabaya ikiwemo kusimama
kwa ujenzi wa miradi.
Kinana amesema hayo leo, baada ya kukagua ujenzi wa kitu kikubwa
cha biashara, katika Kata ya... wilayani Kerwa mkoa ni Kagera ambacho
ujenzi wake umesimama tangu mwaka juzi kwa maelezo ya kukosekana fedha.
"Jamani jengo kama hili lilitakiwa lisimamiwe na Halmashauri ya
eneo hili, lakini kusimamiwa na wizara ni kupoteza muda, hivi kweli ni
rahisi mkaguzi atoke Dar es Salaam, kuja hadi huku kukagua ujenzi tu wa
jengo hili, hasa ikizingatiwa kuwa miradi kama hii ni mingi?" alihoji
Kinana.
Wananchi
wa Kijiji cha Kigorogoro katika Kata ya Murongo wilayani Kyerwa mkoani
Kagera wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCm, Abdulrahman Kinana akipowasili
kuwahutubia mkutano wa hadhara katika kijiji hicho leo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwahutubia Wananchi wa kijiji cha Kibingo Wilayani kyerwa mkoani Kagera.
Wananchi wa kijiji cha Isingiro wakimshangilia Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,alipopanda jukwaani na kuwasalimia.
Wananchi wa kijiji cha Isingiro wakimsikiliza Katibu Mku wa CCM,Ndgu Kinana alipokuwa akiwahutubia.
PICHA NA MICHUZI JR-KYERWA KAGERA.
Tunashukuru kwa ushauri mzuri wa Mh: Kinana, japo bado hata hao Halmashauri wakiachiwa kusimamia miradi nao ni sehemu ya serikali, bado Luna tatizo la watendaji wetu kutokuwa na mapenzi mema kwa nchi yao.
ReplyDelete