Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi waliojitokeza kwenye ofisi za CCM mkoa wa Singida jioni hii ambapo aliwahutubia wananchi na kuwaeleza kuwa huu ni wakati wa kuchagua kiongozi wa kutuongoza hivyo ni vyema wananchi kupima na kuacha ushabiki.
  Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia na Mkuu wa mkoa wa Singida,Dkt.Parseko kone mara baada ya kuwasili mkoani humo na kuwasalimia wananchi akiwa njiani kuelekea mkoani Kagera akiwa ameambatana Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Maofisa wengine wa chama.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na baadhi ya Wanachi wa Mkoa wa Singida jioni hii alipowasili katika ofisi za mkoa za CCM,na pia alipata fusra ya kuwahutubia wananchi,Ndugu Kinana na ujumbe wake wako njiani kuelekea mkoani Kagera kwa ziara ya siku 28. 
 Baadhi ya wafuasi wa Chama cha CCM wakiwa wamekusanyika jioni hii wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana,alipowahutubia kwa muda mfupi nje ya ofis za mkoa wa Singida jioni hii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2015

    Nakubaliana na katibu mkuu wa CCM Nchi hii inahitaji viongozi wanaofaa wenye sifa za kuongoza nchi hii. Kichujio cha vyama kituchujie tupate kiongozi mwenye uwezo kati ya wengi waliojitokeza na watakaojitoteza wapo wenye uwezo, atakayechaguliwa aangalie maslahi ya nchi badala ya kuangalia tumbo lake tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...