MAMA MWASHABAN A. LIGANJA
Miaka (8) inatimia MAMA bila wewe katika maisha yetu ya kila siku, tunakukumbuka daima. UPENDO uliotuonyesha katika maisha ya kila siku mama hatuna la kusema, umetuacha tukiwa bado tunahitaji mawazo yako. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa muda wote uliokuwa nasi.
DAIMA huachwi kukumbukwa na Mumeo George Mapango, wanao Mariam, Eva (Hawa), Jackson, Rose, Patrick (Said) na Richard, Wadogo zako, Kaka zako, Wakwe zako, Marafiki, Wafanyakazi Wenzako pamoja na Wajukuu zako.
Ushauri wako tutaendelea kuufuatilia na mema uliyotufundisha. Daima tutaendelea kukumbuka busara zako na hekima huku tukiwa na tumaini la kuwa siku moja tutaonana nawe.
KISOMO KITAFANYIKA TAREHE 07 JUNI, 2015 SAA 04.00 ASUBUHI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...