Hatimaye siku imewadia, tarehe iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu
kubwa na mashabiki wa taarab wa jiji la Mwanza ndio hii hapa - ni
Mzee Yussuf na Isha Mashauzi katika onyesho la kukata na shoka
ndani ya Villa Park leo usiku.
Ni onyesho linalokutanisha miamba miwili ya taarab ambapo licha ya
kuchukuliwa kama mtu na mwanae lakini upinzani mkubwa
unatarajiwa kutawala katika onyesho hilo lililopewa jina la usiku wa
baba na mwana.
Wasanii wote wawili (Isha na Mzee) wameahidi kumimina uhondo wa
aina yake Alhamisi ya leo hapo Villa Park - Mwanza huku kila mmoja
akikataa kuanika silaha (nyimbo) zake za maangamizi.
Hii ni mara ya kwanza kwa Mzee Yussuf na Isha Mashauzi kukutana
jukwaa moja nje ya Dar es Salaam tangu Isha alipojiengua Jahazi
Modern Taarab ya Mzee Yussuf zaidi ya miaka minne iliyopita.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...