Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Fikiri Juma, pindi alipowasili kwenye Ofisi za CCM Mkoa wa Morogoro, leo Juni 29, 2015 kwa ajili ya kukabidhiwa orodha ya majina ya WanaCCM waliomdhani ili apate ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro, Innocent Kalageris. Mh. Lowassa amehitimisha zoezi hilo la kutafura Wadhamini, leo Juni 29, 2015 katika Mkoa wa Morogoro na amedhaminiwa na WanaCCM 104,038.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akipokea orodha ya majina ya WanaCCM waliomdhani ili apate ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015, kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Kulwa Mironge, leo Juni 29, 2015. Mh. Lowassa amehitimisha zoezi hilo la kutafura Wadhamini, leo Juni 29, 2015 katika Mkoa wa Morogoro na amedhaminiwa na WanaCCM 104,038.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akionyesha fomu yenye orodha ya majina ya wanaCCM waliomdhamini, kwa kadamnasi iliyokuwepo kwenye Uwanja wa CCM Mkoa wa Morogoro, leo Juni 29, 2015, baada ya kukabidhiwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Kulwa Mironge.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza machache na kutoa shukrani kwa WanaCCM waliomdhanini ili apate ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...