Ankal pole na hongera kwa kazi nzuri ya kutupatia taarifa mbali mbali zinazo tuhusu watanzania, napenda kutumia nafasi hii kuomba serikali ya Mh Rais Kikwete iliyopewa dhamana na watanzania kuwaonea huruma watanzania kwakuwapunguzia mzigo mzito wa malipo ya kuingia kwenye maonesho ya SABASABA.
Nimeenda kwenye maonesho hayo lakini nilichoshuhudia jana nikwamba maonesho hayo yamewalenga wenye kipato cha juu tu na si watanzania wakawaida asilani, kwa sababu inashangaza sana kwa serikali kuwakabidhi kampuni ya Maxmalipo kukusanya viingilio tena kwa gharama ya juu sana, Usumbufu mwingine ambao kwakweli auvumiliki, ni kwamba hawa MaxMalipo wanatoza maegesho ya magari kw ash elfu 10, tena wanawafuata hata walio paki nje ya eneo la sabasaba, nakuwalazimisha watu walipia elfu 10 najiuliza hivi hawa wameingia mkataba wakufanya haya na nani asie na huruma na watanzania wenye kipato cha chini?
Nimeshuhudia mzozo mkubwa pale eneo la Jeshini karibu na ATM ya NMB, mteja kaja kutoa pesa kisha wakamlazimisha alipe Tsh elfu 10 kwakuwa ameegesha gari pale, hivi serikali kweli imejiuza kwa hawa MaxMalipo kiasi hicho??? Kwanini mliokabidhiwa mamlaka mnatufanyia hivi walalahoi? Kwanini mnatufanya tushindwe kuingia sabasaba? Mtu huyu anaenda na gari lake tena apaki viwanja vya sabasaba, mnamlazimisha kulipa eflu kumi, kisha alipie elfu 4 getini, mnatutendea haki???? Isitoshe hao vijana wa MAXMALIPO wanakuli mbaya na kuonesha ubabe tena eneo la Jeshi, na nilimsikia mdada mmoja Mjeshi MP aliekuwa zamu mida ya saa nane nane mchana akimlazimisha mtu awalipe MaxMalipo Elfu 10 kwakuwa wanauwalali wakulipwa tozo ya kupaki pale jeshini, hii haikukaa sawa hata kidogo.
Nashauri, Serilika ya Mkoa wa Dar es Salaam, Wizara husika, Jeshi la Wananchi na Mh Rais na CCM chama kilicho iweka serikali Madarakani kuingilia kati suala hili haraka iwezekanavyo, ili kuiepusha serikali kupata sifa mbaya mbele ya wananchi, haiwezekani kukawa na taratibu zisizofaa zinazo wakwaza wananchi wakipato cha chini kuingia kwenye maonesho ya SABASABA, kwanini serikali isidhibiti mapato pale mlangoni au kwenye maegesho kuliko kuingia ubia na mnadu anaeongeza garama zisizo na sababu kwa sisi walalahoi.
Nimatumaini yangu kuwa Serikali hii sikivu ilationa hili na kuwashauri kwa busara walio fanya maamuzi haya ya kumkandamiza mtanzania mwenye shahuku alieituza mwaka mzima ya kwenda Sabasaba kuachana maramoja na msimamo waho huo, maana huko ni nikuendelea kuitengenezea uhasama serikali na wananchi wake hasa tunapoelekea Uchaguzi mkuu.
Ni mimi Mdau wa maonesho ya SABASABA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...