Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Dkt. Kevin Mandopi akizungumza na wadau
mbalimbali wa masuala ya haki za binadamu katika mkutano wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya
Uelimishaji Umma Kuhusu Ualbino uliofanyika kwenye ofisi za Tume hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali Bibi. Neema
Ringo na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bibi. Nkasori Sarakikya.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bibi. Mary Massay akitoa ufafanuzi
kuhusu haki za watu wenye ualbino katika mkutano wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uelimishaji
Umma Kuhusu Ualbino uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bibi. Nkasori Sarakikya.
Mwakilishi wa UNESCO Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza kwenye mkutano wa maadhimisho ya Siku
ya Kimataifa ya Uelimishaji Umma Kuhusu Ualbino leo jijini Dar es Salaam ambapo ameishauri Serikali
kuweka mikakati ya muda mrefu ili kukomesha ukatili na unyanyapaa dhidi ya watu wenye ualbino.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali Bibi. Neema Ringo
(kushoto) akitoa rai kwa watanzania kutoa taarifa mapema za vitendo vya ukatili dhidi ya watu wenye
ualbino katika mkutano wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uelimishaji Umma Kuhusu Ualbino
uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
Dkt. Kevin Mandopi na Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bibi. Nkasori
Sarakikya.
Baadhi ya waandishi wa habari na wadau wa masuala ya haki za binadamu wakifuatilia mkutano wa
maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uelimishaji Umma Kuhusu Ualbino uliofanyika leo jijini Dar es
Salaam.
PICHA ZOTE NA FATMA SALUM - MAELEZO
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...