Ujumbe wa Tanzania unaendelea kushiriki katika kikao cha Mkutano Mkuu wa Kumi na saba wa Shirikia la Hali ya Hewa Duniani (WMO-Congress 17), mijini Geneva, nchini Uswisi. Ujumbe huo umeshiriki katika matukio mbalimbali ya mkutano huo ikiwa ni pamoja na Dkt. Agnes Kijazi kushiriki katika siku ya Jinsia ya WMO (WMO Gender Day), kutoa mada zilizotoa uzoefu wa Tanzania wa utekelezaji wa program za utekelezaji wa programu ya utoaji wa huduma bora za hali ya hewa kwa jamii “Global Framework for Climate Services (GFCS) na programu ya uendelezaji wa mitandao ya upimaji wa hali ya hewa na mawasiliano (WMO Integrated Observation System and WMO Information System-WIGOS/WIS). Kwa habari zaidi angalia picha za matukio mbalimbali ya Mkutano huo hapa.
Balozi wa Tanzania na Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa, Uswiss, Balozi Modest Mero na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Dkt. Agnes Kijazi na Ujumbe wa Tanzania wakishiriki katika Mkutano Mkuu wa Kumi na Saba wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO- Congress-17), Geneva, Uswisi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...