MAELFU ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM, na wakazi wengine wa jiji la Mwanza, leo Ijumaa Juni 5, 2015, walifurika kwa wingi kwenye ofisi za CCM wilaya ya Nayamagana na ile ya Ilemela, wengine wakitaka kumuona na kupeana mikono na wengine kwa nia ya kumdhamini Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edwrad Lowassa, alipofika jijini Mwanza kutafuta wana CCM wa kumdhamini katika safari yake ya Matumaini. (Kuwania urais wa Tanzania kupitia CCM.

Madereva texi, waendesha bodaboda, na hata wafanyakazi na wasafiri kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza, waliacha shughuli zao kwa muda ili walau wamuone mtangaza nia huyo wa nafasi ya jurasi kupitia CCM.

Lowassa alichukua fomu, za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania, Alhamisi Juni 4, 2015 pale makao makuu ya CCM, na safari yake ya kusaka wadhamini ilianza “chap chap” pale pale Dodoma, na Mwanza ndio kituo cha kwanza nje ya Dodoma, ambacho Lowassa, ameanza kampeni yake ya kusaka wadhamini.

Picha ni, Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, ambaye tayari amechukua fomu za kuomba CCM imteue kuwania urais, Edwrad Lowassa, akipungia mkono maelfu ya wanachama wa chama hicho na wananchi wengine baada ya kupata wadhamini kwenye ofisi ya CCM wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza Ijumaa Juni 5, 2015. (Picha na K-VIS MEDIA)
Lowassa, akipokea fomu za wadhamini ambazo tayari zimejazwa na wana CCM wilaya ya Ilemele, kutoka kwa Katibu wa CCM wilayani humo, , Loti Olele Mtui Lazaro.

Watoto wa Chipukizi kutoka Chama Cha Mapinduzi, jijini Mwanza, Marie Kighei Joseph, (wapili kulia) na Sarafina Magabe, wakimkabidhi zawadi ya maua ikiwa ni ishara ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edward Lowasa, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwnza, Ijumaa Juni 5, 2015, ili kuomba wadhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba kuwania urais wa Tanzania kuputia CCM
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2015

    Juzi juzi niliona mgombea urais akichangiwa na wananchi kuchukua fomu. Leo naona mgombea huyo huyo akilipia nauli ya ndege / au kukodisha ndege kwa ajili tu ya kufuata saini za watu. Sasa yule aliyechangiwa na wananchi masikini ana hela za kukodisha ndege? I MISS NYERERE REALLY, I WISH HIS GHOST CAN HELP. I'M ACTUALLY BEGINNING TO MISS KIKWETE TOO. I HATE SOMEONE TAKING ME FOR A FOOL. WHAT'S GOING ON? IS NYERERE'S LEGACY DEAD? WHAT ARE ALL THESE LAVISH EXPENSES FOR? WHO PAYS THEM?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...