Mwanasiasa Mkongwe hapa nchini, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akisani fomu ya udhamini mbele ya Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono mgombea huyo. zoezi hili limefanyika jioni ya leo Juni 27, 2015 kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Kinondoni, Mkwajuni Jijini Dar. ambapo kwa wilaya ya Kinondoni amepata udhamini wa wanaCCM 95, 251 na kufanya jumla kuu kuwa 212, 150 na kuifanya Dar es salaam kuwa Mkoa wa kwanza kuwa na idadi kubwa ya WanaCCM waliomdhamini Mh. Lowassa. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge.




Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza na kuwashukuru wanaCCM wa Wilaya ya Kinondini Jijini Dar es Salaam kwa kumdhamini ili apate ridhaa ya CCM kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Jumla ya WanaCCM 212, 150 wamdhamini Mh. Lowassa jijini Dar.
Katibu wa CCM Wilaya ya Temeke, Robert Kerenge akikabidhi fomu za Wadhamini kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa leo Juni 27, 2015. Jumla ya WanaCCM 72, 100 wa Wilaya ya Temeke Wamemdhamini Mh. Lowassa ili apate ridhaa ya CCM kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza na kuwashukuru wanaCCM wa Wilaya ya Ilala waliomdhamini ili apate ridhaa ya Chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Juni 27, 2015.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ndg. Ramadhan Madabida akizungumza jambo kumuhusu, Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa (kulia), wakati alipofika kwenye Ofisi za CCM Mkoa wa Dar es Salaam kusaini kitabu leo Juni 27, 2015, wakati akiwa katika ziara yake ya kutafuta saini za WanaCCM wakumdhamini ili apate ridhaa ya CCM kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 212, 150 kwa Mkoa wa Dar es Salaam.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...