Wananchi wakiwa wamesimama juu ya daraja la zamani, wakati Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipokagua ujenzi wa daraja jipya la Isegenge katika Kata ya Mahina, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama jimbo la Nyamagana, mkoani Mwanza leo.Ndugu Kinana kesho atahutubia katika mkutano wa hadhara utakaofanyika kwenye viwanja vya Furahisha jijini Mwanza,mkutano huo utarushwa moja kwa moja na televisheni mbalimbali ikiwa ni sehemu ya hitimisho ziara yake ya Mikoa mitatu,kuanzia Mkoa Kagera,Geita na Jijini Mwanza.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua ujenzi wa daraja jipya la Isegenge katika Kata ya Mahina, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama jimbo la Nyamagana, mkoani Mwanza leo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika eneo la soko la Igoma, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama katika jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza leo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na msafara wake wakiondoka katika eneo la mradi wa maji mara baada ya kuukagua na kupata maelezo mafupi juu ya mradi huo wa maji wa Fumagila katika Kata ya Kishiri, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji ilani ya CCM na uhai wa Chama katika jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza leo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza katika mkutano wa hadhara aliofanya baada ya kuzindua Ofisi ya CCM Kata ya Buhongwa, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika jimbo la Nyamagana, mkoani Mwanza leo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, wakati wa uzinduzi Ofisi ya CCM Kata ya Buhongwa, Kinana akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika jimbo la Nyamagana, mkoani Mwanza leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...