Suala la mirathi popote linapotokea hutokea iwapo kuna mtu amekufa na ameacha mali . Mtu akishakufa akaacha mali hata kama hakuna ndugu wa kurithi suala la mirathi lazima liibuke.
Huibuka kwakuwa lazima zile mali ziende pahali iwe kwa mtu au kwa mamlaka.
Hata hivyo suala la mirathi huibua hisia zaidi hasa panapokwa hamna wosia. Marehemu asipoacha wosia lakini akaacha mali mambo huwa sio mepesi sana labda iwe vinginevyo. Ifahamike kuwa mirathi huhusisha mambo mengi. Lakini pia huhusisha sheria nyingi. Sheria za kiislam huhusika, sheria za kimila huhusika na pia sheria za nchi ambayo ni sura ya 352.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...