
Mhariri wa Mwana Halisi
Online, Edson Kamukara (pichani), amefariki Dunia kwa ajali ya moto nyumbani
kwake Mabibo jijini Dar es Salaam leo hii majira ya saa moja kasorobo jioni,
baada ya kulipukiwa na jiko la gesi, habari zilizotufikia sasa hivi zinasema kuwa
Polisi wameuchukua mwili wa marehemu na kwenda kuhifadhi katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi wa kifo chake.
Ofisa Uhusiano wa NMB, Viccent
Mnyanyika akimkabidhi zawadi marehemu Edson Kamukara wakati wa uhai wake kwenye
wa utoaji wa tuzo za Umahiri za Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT)
zilizofanyika Aprili 24 mwaka huu.
Globu ya Jamii inaungana na familia ya marehemu, ndugu, jamaa, wafanyakazi wenzake, marafiki na majirani katika msiba huu. Mola na aiweke mahala pema Roho ya Marehemu,
AMINA
Poleni sana wafiwa, so young and gone too soon!!
ReplyDeleteJe tunatakiwa kuboresha usalama na viwango vya majiko au mitungi ya gesi inayotumika, tukio hili lakusikitisha litusukume pia kuangalia swala hilo pia, au ilikuwa tu ajali?.
ReplyDelete