Mtangaza nia kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao Charles Makongoro Nyerere leo amekamilisha ziara ya  kutafuta wadhamini mikoani.Ziara yake ameikamilisha katika mkoa wa Shinyanga.Katika hotuba yake ya kukamilisha ziara yake,Makongoro Nyerere amekemea vitendo vya mafisadi aliodai hawazidi 20,anaowafahamu sura,majina na tabia zao ambao wamekuwa kikwazo hata kwa rais Jakaya Mrisho Kikwete,aliodai kuwa wengi ni marafiki zake na rais.
 
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangura akikabidhi fomu ya majina ya wadhamini wa mtia nia ya urais Makongoro Nyerere
Makongoro Nyerere akishikana mkono na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu Tajiri Maulid
Makongoro Nyerere akionesha mkoba uliobeba Fomu zake baada ya kukamilisha zoezi la kupata wadhamini na kuelekea Dodoma kwa ajili ya kukabidhi fomu hizo makao makuu na kubiri jina lake lipitishwe na kikao cha halmashauri kuu ya CCM Julai,12 mwaka huu. Mwandishi Kadama Malunde, ametuletea hizi picha na h0tuba ya Mhe Makongoro BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...