Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kushoto akikabidhiwa fomu yenye orodha ya
Wadhamini waliojitokeza kumdhamini katika
mbio za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama
cha Mapinduzi CCM kutoka kwa Katibu wa
CCM Wilaya ya Morogoro mjini
Dkt. Magufuli akiangalia
kwa makini zoezi la uhakiki wa Wanachama na udhamini likiendelea katika Ofisi
za CCM Wilaya ya Morogoro mjini.
Katibu wa Chama cha
Mapinduzi CCM Wilaya ya Morogoro Mjini akikagua kadi za wanachama waliojitokeza
kumdhamini Waziri Magufuli.
. Waziri wa Ujenzi Dkt.
John Magufuli akinyoosha juu fomu zake za wadhamini walijitokeza kumdhamini
katika Mkoa wa Morogoro.
Dkt. Magufuli akisalimiana
na baadhi ya Wanachama wa CCM mkoani Morogoro waliojitokeza kumdhamini.
Vijana wa Morogoro
wakimshangilia Waziri Magufuli mara baada ya kutoka kwenye Ofisi za CCM Wilaya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...