Mkurugenzi wa kampuni Exclusive media, Gody Gervas akizungumza na waandishi wa habari leo katika Hoteli ya Kebbys jijiji Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Qutub Global Ltd,Jeremia Fumbe na kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Exclusive media (T)Ltd ESunday Mashele.
Na Avila
Kakingo,Globu ya Jamii.
KAMPUNI Exclusive
media (T)Ltd ikishirikiana na Qutub Global Ltd kukutanisha Tasisi na Asasi za
Kifedha hapa nchini katika maonyesho ya Pesa
Expo katika Maonyesho yatafanyika mwanzoni wa mwezi Septemba mwaka huu.
Hayo yamesemwa
na Mkurugenzi wa kampuni Exclusive media, Gody Gervas wakati akizungumza na
waandishi wa habari katika Hoteli ya Kebbys jijiji Dar es Salaam leo.
Gervas amesema Pesa Expo itahusiaha baadhi ya
taasisi za kifedha ambazo zinaweza kushiriki katika maonyesho hayo ni pamoja na
Mabenki, Saccos,Makampuni ya Bima, Makampuni yanayotoa huduma za mikopo,makampuni
yanayotoa huduma za fedha za kieletroniki, Mifuko ya hifadhi ya jamii,
Makampuni yanayotoa huduma za kutuma fedha,Soko la hisa na madalali wake,Makampuni
yanayotoa huduma za ushauri wa kifedha na Taasisi zisizo na faida zinazotoa
elimu kuhusu mambo ya fedha.
Gervas
ameongeza kuwa makampuni ambayo hayaja
thibitisha ushiriki katik maonyesho hayo wadhibitishe ili kuwapa elimu wananchi
kuhusiana na huduma nyingi za kifedha
zinazotolewa hapa nchini.
Amesongeza kuwa
makampuni yatakayoshiriki katika
maonyesho hayo ni kufanya mauzo ya moja kwa moja, kutangaza huduma zao mpya,
kutoa elimu ya huduma kwa wananchi, kuboresha mahusiano baina ya makampuni
shiriki,kubadilishana mawazo na wajasiliamali na
wananchi,kufanya tafiti ya
bidhaa zao pamoja na kujitangaza.
Maonyesho hayo
ya Pesa Expo yataanzia jijini Dar es
Salaam na baadae mikoa mingine.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...