Afisa wa wa Wakala wa Usajili,ufilisi na udhamini(RITA), Joseph Mwakatobe akizungumza na Michuzi TV juu ya huduma
wanazozitoa katika huduma ya Wosia katika kuondoa migogoro ya miradhi
wakiwa katika maonyesho Wiki ya Utumishi inayoendelea katika Viwanja
vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Shughuli za Maafa Idara ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu,Edgar Senga akizungumza na Michuzi TV juu ya huduma za Mafaa wanavyotoa inapotokea majanga na kutaka
wananchi wajue shughuli hizo zinazotolewa na kitengo hicho katika maadhimisho
ya Wiki ya Utumishi wa umma yanayoendelea katika
Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Msaidizi
wa Ofisi ya Kitengo cha Uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu,Lylian Mmari
akitoa maelezo kwa mteja alipotembelea banda la ofisi ya Waziri Mkuu
katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa umma yanayoendelea katika Viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa ofisi ya Waziri Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja katika
banda la Waziri Mkuu katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Kiongozi Mkuu na Mratibu wa Sayansi na Maendeleo ya Milleniam
Vijijini katika kuondoa Umasikini ,Dk.Gerson Nyadzi akizungumza na
Michuzi TV katika Banda la Wizara ya Fedha juu ya wananchi walivyoweza
kunufaika na miradi mbalimbali katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi
wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es
Salaam.
Afisa wa Wizara ya Fedha akitoa maelekezo kwa mteja aliopotembelea banda
la Wizara ya fedha katika maaonyesho ya wiki ya utumishi wa Umma
yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mhasibu wa Wizara ya Fedha Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali
,Kitengo cha Pensheni,Emelda Mzatulla akizungumza na Michuzi TV juu ya
huduma wanazozitoa katika kitengo cha pensheni katika Wiki ya Utumishi
inayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...