Mgeni rasmi katika mchezo wa robo fainali ya Netiboli kati ya Mtwara dhidi ya Mwanza Bibi Odilio Mushi ambaye pia ni Afisa Elimu Mkuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI akitoa nasaha kwa wanamichezo hao mara baada ya kuzikagua timu zao katika viwanja vya Chuo cha Ualimu cha Butimba, Mwanza.
Waamuzi wa mchezo wa riadha wanaoshiriki katika mashindano ya UMITASHUMTA wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufanyika kwa fainali ya mbio za mita 400 yanayoendelea katika viwanja vya Chuo cha Ualimu cha Butimba, Mwanza.
-------------------------------------------------
Matokeo ya mpira wa miguu kwa
wavulana yanaonyesha kuwa Ruvuma na Katavi
zilitoka sare ya 1-1, Tanga walifungwa na Rukwa 2-1, huku Kilimanjaro ilitoka sare ya 1-1 na
Tabora. Pia Shinyanga iliifunga pwani 1-0, Kigoma iliifunga Iringa mabao 2-0
huku Mbeya ikaibamiza Manyara 4-0.
Matokeo ya mpira wa wavu kwa
wavulana yanaonyesha kuwaMtwara ilishinda Mara kwa seti 2-0, Mwanza ikaichapa
Shinyanga seti 2-0, Manyara ikaishinda Tabora seti 2-0, na Ruvuma ikaichabanga
Kilimanjaro seti 2-0.
Kwa upande wa wasichana Tanga
ikaifunga Shinyanga seti 2-0, Mtwara iliichabanga Manyara seti 2-0, Kigoma
iliifunga Singida seti 2-0 na Katavi iliilaza Simiyu seti 2-0.
Katika mpira wa mikono kwa
wavulana Rukwa iliichapa Manyara mabao 15-10, Dar es salaam iliichapa na Tabora
mabao 31-11, Singida ilifungwa na Mwanza mabao 20-5, ma Morogoro iliifunga
Kigoma mabao 15-8.
Katika mchezo wa mpira wa mikono
wasichana, Geita iliichapa Tabora mabao 24-6, Pwani iliifunga Iringa mabao 7-5,
huku timu za Mbeya na Lindi zilitoka sare mabao 11-11m na Tanga iliichabanga
Manyara mabao 11-2.
Kwa upande wa mpira wa Netiboli, Arusha
iliifungaSimiyu mabao 29-13, Katavi
ilifungwa na Morogoro mabao 36-18, Mbeya iliichakaza Manyara mabao 31-16,
Dodoma iliifunga Singida mabao 21-12 na Lindi iliilaza Kigoma mabao 38-36.
Matokeo ya mpira wa kengele kwa
wavulana yanaonyesha Mtwara iliifunga Mbeya mabao 11-3, Kilimanjaro iliifunga
Singida mabao 8-5, Dodoma ilifungwa na Kagera mabao 9-11 na Manyara iliifunga
Tabora mabao 5-2.
Kwa upande wa mpira wa kengele
wasichana Kilimanjaro iliifunga Singida mabao 10-3 na Kagera iliilaza Tabora
mabao 9-4.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...