JAMII imeombwa kutoa msaada wa hali na mali kwa BI GRACE KAIZA mkazi wa Igoma jijini Mwanza ambaye ameomba mukatwa mguu wake kutokana na Saratani ( Kansa) katika mguu huo.
Akizungumza na *JEMBE Habari* Bi. Grace Kaiza amesema amekuwa akisumbuliwa na maradhi hayo kwa muda mrefu jambo lililomuathiri kwa kiasi kikubwa kiafya na hata kiuchumi.
Akielezea namna tatizo hilo lilivyompata amesema lilianza kama uvimbe katika mguu wake kisha kufanyiwa upasuaji mara kadhaa lakini haikusaidia na ndipo alipobainika kuwa na ugonjwa huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...