Mbunge wa jimbo la Kalenga Wilaya ya Iringa mkoani Iringa Bw Godfrey Mgimwa.

MBUNGE wa jimbo la kalenga Wilaya ya Iringa mkoani Iringa Bw Godfrey Mgimwa ametoa msaada wa bati 50 na vitu mbali mbali vyote Vikiwa na thamani ya zaidi ya Tsh milioni 3.5 kwa ajili ya watoto yatima wa kituo cha Tosamaganga kata y a Kalenga.

Mbunge huyo amekabidhi msaada leo Mbunge Mgimwa alisema kuwa amelazimika kutoa msaada huo kama sehemu ya kuhamasisha jamii hapa nchini kujenga utamaduni ya kusaidia watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu.

Alisema kuwa kituo hicho cha yatima ni moja Kati ya vituo vya yatima vyenye historia kubwa katika jimbo hilo hasa kutokana na utaratibu wake wa kupokea watoto kutoka maeneo mbali mbali ya jimbo la kalenga na Mkoa mzima wa Iringa.

Hivyo alisema kwa upande wake bado anawaomba wadau mbali mbali kuendelea kusaidia watoto hao yatima.

Pia alisema akiwa kama mbunge wa jimbo hilo hatapenda kuona yatima wanasaidia pia maendeleo ya jimbo hilo yakizidi kusonga mbele.

Diwani wa kata ya Kalenga   Bi Emeliana Galinoma pamoja na kumshukuru mbunge Mgimwa kwa msaada huo kwa watoto hao yatima bado alisema kuwa kwa jimbo hilo la Kalenga limepata kuwa na wabunge zaidi ya watano sasa ila jitihada za mbunge Kijana Mgimwa zimeonekana ndani ya mwaka mmoja.

Bi Galinoma alisema kuwa kwa sasa wananchi wa kalenga hawahitaji kuwa na mbunge zaidi ya Mgimwa na kuwa kipimo cha utendaji wake tayari wameona ndani ya mwaka mmoja toka alipochaguliwa baada ya mbunge aliyechaguliwa mwaka 2010 kutangulia mbele za haki.

"Tumekuwa tukibadili wabunge kila baada ya miaka mitano na ukweli kila mbunge amekuwa akifanya Kazi kulingana na changamoto za wakati huo ila kwa kipimo cha mwaka mmoja ambacho amepata kuwepo madarakani mbunge Mgimwa kuna Kazi kubwa ameionyesha"

Diwani Bi Galimoma ambae alikuwa ni mke wa mbunge wa zamani wa Kalenga marehemu Steven Galinoma alisema mbali ya kuwa mwaka huu hagombei tena udiwani ila ataungana na wananchi wa jimbo la kalenga  kuona mbunge mgimwa anaendelea kuwa mbunge tena.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...