Waziri wa Fedha Mh. Saada M.Salum(MB) akiwa katika mgahawa wa Dodoma Carnival alipotembelea kukagua matumizi ya mashine za EFD. Mh.Waziri aliagiza mgahawa huo ufungwe mpaka hapo watakaponunua mashine hizo. Kushoto kwa Mh.Waziri ni meneja wa TRA Mkoa wa Dodoma na mwenye shati jekundu ni msimamizi wa mgahawa huo.

Mh.Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (MB) akijadiliana jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha Bi.Ingiahedi Mduma mara baada ya kufanya ukaguzi wa matumizi ya mashine za EFD katika duka mojawapo Mkoani Dodoma
.……………………………………….
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum amefanya ukaguzi wa ghafla katika baadhi ya maduka Mkoani Dodoma ili kuona kama maelekezo ya Serikali kuhusu matumizi ya mashine za EFD yanatekelezwa ipasavyo.
Katika ukaguzi huo ambao ulihusisha maduka ya kuuza thamani za majumbani,nguo na maduka ya kuuza bidhaa mchanganyiko (Mini supermarket).
Mh.Waziri akiongozana na Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania aliagiza kufungwa kwa maduka yote ambayo yamekaidi agizo la Serikali la matumizi ya mashine EFD mpaka pale watakaponunua na kuzitumia ipasavyo mashine hizo.
Aidha Mh.Waziri amewataka wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kuisaidia Serikali kuwafichua wafanyabiashara wasio waaminifu na ambao wanapelekea kuikosesha Serikali mapato ambayo yangetumika katika kuboresha huduma za kijamii.
Imetolewa na Msemaji Mkuu,
Wizara ya Fedha
Dodoma
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...