WATANZANIA wametakiwa kuwatumia wasanii katika kufikisha ujumbe wa masuala muhimu ya kijamii kwakuwa wasanii hao wanamvuto mkubwa kwa wananchi.
Hayo yalisema jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa wimbo maalum wa kuhamasisha utunzaji wa mazingira  uliojulikana kama  ‘Mkuhumi’.

Wimbo huo ulioimbwa na wanamuziki wa kizazi kipya Seleman Msindi ‘Afande Sele’, Dayna Nyange pamoja na msanii nguli wa kughani mashairi Afrika Mashariki, Mrisho Mpoto maarufu kama ‘Mjomba’.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa wimbo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu nchini (Mjumita), Rahima Njaidi alisema, wameamua kuwatumia wasanii hao kwa kuwa ni rahisi kufikisha ujumbe kwa jamii.
Alisema lengo kuu la wimbo huo ni kuwahamasisha wananchi kutunza mazingira ili waweze kunufaika na Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana na ukataji na uharibifu wa Misitu (Mkuhumi), kupitia fedha zinazotolewa na nchi zenye viwanda.

“Watu wengi tunapoenda kusikiliza muziki kuliko kusoma, kwa maana hiyo kama tungeweka elimu hii kwenye vipeperushi isingekuwa rahisi kwa watu wote kupata ujumbe, lakini tunategemea kupitia muziki huu tutawafgikia watu wengi,” alisema.

Alisema wimbo huo umetayarishwa chini ya usimamizi wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Mkuhumi ili kuwafikia wadau ili kwa pamoja waweze kuchukua tahadhari na kupunguza shughuli zinazochangia kutokea kwa mabadiliko ya tabia nchi.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...