Maandalizi ya kutandaza mkeka wa uhakika katika Barabara ya kutokea Hedaru mpaka Same mkoani Kilimanjaro umekuwa ukienda vyema kadri siku zinavyokwenda na kuleta matumaini ya safari njema na ya uhakika kwa watumiani wa barabara hiyo, pichani ni moja ya gari likipita kwenye barabara ya muda wakati mkema wa ukweli ukiendelea kutandandazwa.
Mafundi wa Ujenzi wa barabara hiyo wakiendela na kazi, ili kuhakikisha mkeka wa uhakika unapatikana haraka iwezekanavyo.
Sehemu ya mchekupuko.
Muonekano wa barabara ya zamani huku ya muda ikiendelea kuandaliwa.
Ili kupatikana mkeka ulio bora, ni lazima umwagiliaji uhusike.
Mmoja wa wataalam wa Ujenzi wa barabara hiyo akipitia nyuzzzzz....
Kazi kubwa imefanyika ya ujenzi wa barabara tuendelee na kazi nzuri hii.
ReplyDeleteNilipita barabara ya Bukoba Karagwe ilipokuwa ni mbaya sana miaka ya nyuma wakati huu lori za kahawa tu ndiyo zilikuwa zinatumika zaidi,kufika ilikuwa inatumia muda mrefu, nikapita wakati msamaha wa madeni umeiwezesha barabara hii kupitika kwa wakati wote ikawa afadhali. Baadaye lami ikawa mpaka Kyaka, sasa lami mpaka Bugene, safari imekuwa fupi, maendeleo yapo.
ReplyDeleteCCM yajenga Nchi
ReplyDeleteTango Mike - Arusha
Nadhani katika eneo ambalo utawala huu unaweza kujivunia pasipo shaka ni ujenzi wa miundo mbinu ya barabara. .
ReplyDelete