Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
MAMLAKA ya chakula na dawa wamewataka wananchi kuepukana na kutumia bidhaa za vipodozi feki , kwani bidhaa hizo zina madhara makubwa kwa mtumiaji.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Usajili wa vipodozi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Grace Shimela wakati wa uzinduzi kipodozi aina ya Manjano Luvtouch katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam jana.
Shimela alisema kuwa wamiliki wote wa bidhaa vya vipodozi wanatakiwa kusajili bidhaa zao ili wafanye biashara kwa uhuru kuliko kukimbiza na wakaguaji wa bidhaa na mamlaka ya chakula na dawa.
Nae Mwasisi wa Manjano Foundation na Mmiliki wa Shear Illusions,Shekha Nasser alisema kuwa kipodozi cha Luvtouch Manjano ni kipodozi kinachotumika na rika zote awe mzee au kijana, pia kinatumika kwa wakati wa joto au baridi na ambapo kinahitajika.
Pia aliongezea kuwa ameona wanawake wengi wakitumia vipodozi kwa kutokuzingatia wakati unaofaa, wengi hutumia vipodozi kwa wakati usiofaa kama kipodozi cha ofisini ni tofauti na sehemu ya sherehe.
“Huu ni wakati wa kila mwanamke kujiremba jinsi awezavyo kutokana na vipodozi kupatikana hapahapa nchini ikiwa vipodozi vingi vimekuwa vikiwaharibu wanawake ila kwa hiki kinafaa kwa kwa ngozi zetu”alisema Shekha Nasser.
Meneja wa Usajili wa vipodozi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Grace Shimela akimkabidhi jarida ambalo linaonyesha matumizi mbalimbali ya Manjano Luvtouch Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda katika uzinduzi wa Manjano,uliofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam jana.

Mwazilishi
wa Manjano Foundation na Mmiliki wa Shear Illusions,Shekha Nasser
akielezea jinsi bidhaa ya manjano foundation ilivyo nzuri kwa
ngozi katika uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa Diamond
Jubilee,jijini Dar es Salaam jana.
Meneja
wa Usajili wa vipodozi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Grace
Shimela akizungumza katika uzinduzi wa Manjano foundation akizungumza
katika uzinduzi wa bidhaa ya Luvtouch katika uzinduzi uliofanyika katika
ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam jana.
Mke
wa Waziri Mkuu,Tunu Pinda alimpaka bidhaa ya Manjano Luvtoach katika
Uzinduzi wa Manjano Foundation na bidhaa za Luvtouch iliyofanyika katika
Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya watu walioshiriki katika uzinduzi wa bidhaa ya manjano Foundation katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam jana.
PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.
Wanawake wajirembe lakini wasitumie vipodozi hatarishi, weusi wa wengi ni mzuri hakuna haja ya kujichubua au kuweka make up nyingi. Tusisahau black is beauty au I am black and proud.
ReplyDelete