Na Avila kakingo,Globu ya Jamii.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi amewaagiza watendaji na wataalamu na wenye elimu ya utunzaji wa Mazingira kutoa elimu kuhusu utunzanzaji wa mazingira na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi kwa wananchi wote.

Akizungumza leo na Waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo,Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi amesema kuwa katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki ndiye Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Wiki ya mazingira yatakayofanyika katika viwanja vya kawe jijini Dar es Salaam.

Mushi ametoa wito kwa wananchi wote kujitokeza katika kufanya usafi wa mazingira yao wanayoishi bila kushurutishwa na kwa matumizi endelevu, ikiwa kauli mbiu ya mwaka huu katika maadhimisho ya Mazingira Duniani ni "Ndoto billioni saba, Dunia moja,tumia Raslimali kwa uangalifu"

Amesema kuwa manispaa ya Ilala imetawaliwa na eneo kubwa la mji ambalo siku hadi siku kunaongezeko kubwa la ujenzi wa majumba ya kibiashara,makazi na viwanda hali hii inaongeza uchafunzi wa mazingira kwa kiwango kikubwa hivyo wananchi wanashauriwa kufanya tathmini ya adhario ya mazingira.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam,kuhusiana na uzinduzi wa siku ya mazingira Duniani itakayofanyika 5 June  mwaka huu yatakayofanyika viwanja vya kawe jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi akizikiliza Swali kutoka kwa mwandishi wa habari leo ofisini kwake kuhusiana na siku ya mazingira duniani itakayofanyika jijini Dar es Salaam Juni 5 mwaka huu,katika viwanja vya Kawe jijini Dar es salaam.Picha na Avila Kakaingo,Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 02, 2015

    Tukitunza mazingira vema vizazi vijavyo vitakuta raslimali za kutosha zitakazowezesha maisha yao. Kata mti panda miti mitano. Usikae katika maeneo yenye mazingira hatarishi kwa maisha yako.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...