Zimekusanywa na
Samuel Kamugisha
CHANNEL 10
*Baraza la Taifa la elimu ya ufundi NACTE lafuta usajili wa vyuo 3 na 16 kushushwa hadhi katika jitihada za kulinda ubora wa elimu nchini. http://youtu.be/2HosRmHz7lU
*Jaji Augustino Ramadhani apata wadhamini mkoani Kilimanjaro huku akisema endapo atachaguliwa atashirikiana na wagombea wenziwe. http://youtu.be/qU7V9hQfIlI
*Kada wa CCM Edward Lowassa asema hababaishwi na kashfa,vitisho na matusi anavyokumbana navyo kwani ana nia ya dhati ya kuongoza taifa. http://youtu.be/E3B2b4y_uiQ
*Chama cha Mapinduzi Zanzibar kimesema kitendo cha wajumbe na mawaziri wa CUF kususia kikao cha Bajeti ni kinyume cha Katiba. http://youtu.be/2UiljpCNCho
*Jaji mkuu Othman Chande azindua majarida ya sheria yanayo husu maamuzi ama hukumu za mahakama kuu ikiwa ni mara ya kwanza nchini. http://youtu.be/pvJ_xL6GZD4
*Kituo cha sheria na haki za binadamu kimezindua taarifa ya haki za binadamu na biashara 2014 huku ikionyesha ukiukwaji mkubwa wa haki. http://youtu.be/VtNbOW6H3tM
*Wananchi wilayani Misungwi waiomba serikali msaada wa chakula kufuatia njaa katika wilaya hiyo baada ya mvua kusomba chakula chao. http://youtu.be/gYD1YcRD6uA
STAR TV NEWS
*Raisi Kikwete ataka Tanzania kutondokana na utegemezi huku akitaka raisi ajaye kuwekeza mageuzi makubwa ya sayansi na teknolojia. http://youtu.be/zRVrFA5SunQ
*Dr. Mwele Malecela awataka wanawake nchini kutumia fursa ya uchaguzi mkuu ujao kuhakikisha wanawania uongozi ili kuwa miongoni mwa vyombo vya maamuzi nchini. http://youtu.be/XJBQMYwTJRM
*Ajali ya moto yatokea katika msikiti wa Masjid Omar jijini Dar es salaam huku sheikh wa msikiti huo akiwataka waumini wake kuwa watulivu. http://youtu.be/qlm9AeNgQGA
*Njia mpya ya utalii yabuniwa nchini itakayo wafanya watembelee vituo mbalimbali ya asili nchini.http://youtu.be/m41j6KgBbmU
AZAM TV NEWS
*Madaktari wasema mavazi aina ya skin Jeans yanaharibu misuli na mishipa ya damu hivyo kuleta madhara kiafya.http://youtu.be/72C-dyJvjLI
*Vijana washauriwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha BVR ili kupata fursa ya kuchagua viongozi wanao wahitaji .http://youtu.be/bHPSBbD9ozU
*Wazee wasiojiweza na walemavu mkoani Mwanza wanakabiliwa na hali ngumu ya kimaisha baada ya Mzabuni kusitisha utoaji huduma kwa wazee hao kwa kinachodaiwa kuwa deni kubwa. http://youtu.be/12_tDsCctXw
TBC NEWS
*Watu 6 wakiwemo raia 3 wa Kenya watiwa mbaroni mkoani Mara kwa kosa la kujaribu kuvuruga zoezi la uandikishaji wapiga kura BVR. http://youtu.be/uGcO0gnyNVo
*Jeshi la polisi Mkoani Manyara linawashikilia watu 3 kwa tuhuma za kujiandikisha mara mbili katika daftari la wapiga kura.http://youtu.be/G9BOu7RITL0
*Chama cha Mapinduzi kimeishauri serikali kurejesha mswada wa habari kwa wadau wa habari kabla ya kuupeleka bungeni ili kuweze kupatika muafaka. http://youtu.be/PGkhpqD-dxg
*Kamati kuu ya CCM inatarajiwa kukutana mwishoni mwa wiki hii mjini Dodoma chini ya mwenyekiti wake Dr.Jakaya Mrisho Kikwete. http://youtu.be/Skg38Hrx0r4
This is a good move...inatuwezesha tulio nje ya nchi kupata summary ya news za nyumbani Tanzania. Big up Simu TV
ReplyDelete