THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425 |
|
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE
HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Kikwete aanza ziara ya nchi tatu Ulaya.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,
Jumatatu, Juni Mosi, 2015 ameanza ziara rasmi ya wiki moja katika nchi tatu za
Ulaya kwa mwaliko wa viongozi wa nchi hizo.
Rais
Kikwete ambaye aliondoka nchini usiku wa jana, Jumapili, Mei 31, 2013 baada ya
kumaliza kuendesha Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuia ya Afrika
Mashariki (EAC) kuhusu Burundi ameanzia ziara yake katika Finland ambako atakaa
kwa siku tatu.
Baadaye,
Rais Kikwete atatembelea nchi za Sweden na Uholanzi kabla ya kurejea nyumbani.
Katika
Finland, Rais Kikwete miongoni mwa mambo mengine kesho Jumanne, Juni 2, 2015,
atafanya mazungumzo rasmi ya Kiserikali na Rais wa nchi hiyo na baadaye
atatembelea Bunge la nchi hiyo ambako atafanya mazungumzo na Wabunge.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
1 Juni, 2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...