MWANDISHI wa habari mwandamizi wa Shirika la Utangazaji nchini TBC FLORENCY DYAULI (Pichani enzi za uhai wake)amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua.
FRORENCE DYAULI amefariki dunia majira ya saa kumi alfajiri akiwa amelazwa katika hospitali ya RABININSIA MEMORIAL jijini Dar es Salaam, ambako alikuwa akipata matibabu.
Dyauli alizaliwa tarehe 27 mwezi wa saba mwaka 1961 na amefariki dunia tarehe 18/06/2015.
Marehemu DYAULI alisoma shule ya msingi CHANG’OMBE mwaka 1968 hadi 1975.
Alipata elimu ya sekondari mwa 1976 hadi 1979 katika shule ya wasichana KISUTU jijijini Dar es Salaam.
Baadae alijiunga na Chuo cha Uhazili TABORA na kupata cheti katika fani ya katibu muhtasi mwaka 1980 hadi 1981.
Marehemu DYAULI alipata stashahada ya uandishi wa habari mwaka 1988 katika chuo cha Uandishi wa habari TSJ jijini Dar es Salaam.
Taratibu za mipango ya mazishi tutaendelea kuwajulisha katika taarifa zetu zijazo.
Poleni sana kwa msiba mkubwa uliyowapata Mungu amlaze mahali pepa poponi. Amina
ReplyDeletemary kahabuka