Watanzania wanaoishi UAE, Dubai wameanda mechi kati ya Simba na Yanga Mtani jadi ambayo itaitwa "Union Cup Bonanza" ambapo mgeni rasmi atakuwa balozi wa Tanzania huko United Arab Emirates kutoka Abu Dhabi. 
Mechi itapigwa kwenye uwanja wa Al Ahly uliopo Dubai saa tatu usiku za huko, wachezaji wa timu zote mbili wanachezea timu ya watanzania wanaoishi UAE ambayo inajulikana kwa jina "TanzaniaTeamInUAE" 
Baada ya mechi kuisha mshindi atakabidhiwa zawadi na kikombe na wageni watapata nafasi ya kula chakula cha usiku pamoja na wachezaji, timu hiyo pia kwa mara ya kwanza inatarajiwa kushiriki ligi inayofanyika kwenye mwezi wa Ramadhan ambapo timu kutoka nchi mbali mbali zinashiriki kwenye ligi hiyo 
 Mashabiki wengi kutoka miji mbali mbali wanatarajiwa kuhudhuria kwenye mechi hiyo iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na inategemea kuwa na ushindani mkubwa
 Kikosi cha Simba Abu Dhabi
Kikosi cha Yanga Abu Dhabi
 Yanga na Simba
Kikosi cha Yanga mazoezini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...