TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI - RELEASE NO. 15
JUMLA ya miradi 13 yenye thamani ya Zaidi
ya shilingi milioni 1.2 inatarajiwa
kuzinduliwa pamoja na kuwekwa mawe ya msingi na Mwenge wa uhuru utakapokimbizwa
katika Halmashauri ya wilaya ya Mufindi mapema alhamisi ya tarehe 25 mwezi huu.
Taarifa
ya Ofisi ya habari na mawasiliano ya halmashauri ya Mufindi kwa vyombo vya
habari imefafanua kuwa, vyanzo vya fedha zilizotumika kukamilisha miradi
hiyo vimegawanyika katika sehemu kuu
nne, ambapo asilimia 10 ya fedha
hizo ni kutoka serikali kuu, asilimia 12
ni Fedha za Halmashauri, wakati asilimia 13 ni fedha za wahisani huku
wananchi wakichangia asilimia 65.
Taarifa hiyo imeendelea kubainisha kuwa miradi
hiyo 13 imegawanyika katika vijiji
vya Mtili, Lugolofu, Mabaoni, Idetelo, Lugongo na kata ya Kinyanambo huku
miradi mikubwa Zaidi ni pamoja na mradi wa sakosi ya Faraja wenye gharama ya
Zaidi ya sh milioni 478
utakaozinduliwa katika kata ya Kinyanambo sanjari na mradi wa msitu ulioghalim
Zaidi ya Sh. Milioni 180 utakao
kaguliwa katika kijiji cha Lugongo.
Aidha,
Mwenge wa uhuru utakabidhiwa kwa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi, katika hafla
itakayo fanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari Kinyanambo majira ya saa
mbili asubuhi, ukitokea Manispaa ya Iringa na badaye jioni utakesha katika
kijiji cha Mabaoni Mgololo kata ya Makungu.
Mwenge
wa uhuru uliasisiwa rasmi mnamo mwaka 1960
na hayati Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Nyerere, ukiwa na shabaha ya kuleta matumaini, upendo, heshima na
kuchochea maendele katika jamii za kitanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...