Na.
Andrew Chimesela
Mwenge wa uhuru ambao kwa sasa uko
Mkoani Morogoro, umepitia miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo mradi wa maji
uliogharimu shilingi 555,227,710.40 na unatazamiwa
kuwapatia maji safi na salama wananchi
10,534 ambao ni wakazi wa kijiji cha Kibedya Wilayani Gairo.
Mwenge huo ambao umeingia siku
yake ya pili, tangu kuwasili Mkoani
Morogoro ukitokea Mkoani Tanga, na kukimbizwa Wilaya ya Mvomero, Leo ukiwa
Wilayani Gairo umefungua mradi wa maji wenye matenki mawili yenye jumla ya lita
za ujazo 180,000.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa
kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Bw. Juma Khatib Chum, muda mfupi kabla kuufungua,
ilielezwa kuwa mradi wa maji wa Kibedya uliibuliwa na wananchi na kuingizwa
kwenye program ya Serikali ya miradi ya maji ya vijiji kumi Wilayani Gairo.
Mradi wa Maji wa Kibedya umejengwa
kwa ufadhili wa Benki ya Dunia kupitia mpango wa maendeleo ya Sekta ya Maji, na
wananchi kuchangia ardhi ulipojengwa mradi huo yenye thamani ya shilingi 1,500,000,.00.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa lengo
mahsusa la mradi huo ni kuwapatia wananchi wa Kijiji cha Kibedya maji safi na
salama hali itakayochangia kuboresha maisha yao kwa kupata muda wa kutosha
kufanya shughuli nyingine za kiuchumi badala ya kutumia muda huo kutafuta maji.
Naye Kiongozi wa Mbio za Mwenge
Kitaifa Juma Khatib Chum baada ya kuufungua, mradi huo, aliwataka wananchi wa
Kijiji cha kibedya kuuendeleza na kuutunza mradi huo ili uweze kudumu kwa muda
mrefu.
“ Ninawasihi wananchi wa Kijiji
cha Kibedya kuendeleza na kutunza
miundombinu ya mradi huu pamoja na vyanzo vyake vya maji ili mradi udumu kwa
muda mrefu na kuja kunufaisha vizazi vingine vijavyo” alisema.
Mwenge wa uhuru leo umekimbizwa
katika Wilaya ya Gairo ambapo umepitia jumla ya miradi ya maendeleo sita, yenye
thamani ya shilingi, 905,071,355.40.
Hiyo ikiwa ni pamoja na mchanggo
kutoka Serikali Kuu ni shilingi 715,390,635.40, mchango kutoka Halmashauri ya
Gairo shilingi 7,578,720.00, nguvu za wananchi silingi 180,387,000.00 na
wahisani walichangia shilingi 1,715,000.00.
Mwenge wa Uhuru kesho utakimbizwa
katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Ndugu Juma
Chum akifungua mradi wa maji wa Kijiji cha Kibedya Wilayani Gairo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...