Na Mwandishi Maalum, New York 
 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Ecuador zimekubaliana kuanzisha uhusiano wa kudiplomasia katika ngazi ya Mabalozi . Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, na Mwakilishi wa Kudumu wa Ecuador katika Umoja wa Mataifa Balozi Xavier Mendoza ndio waliotia sahihi hati za kuanzishwa kwa uhusiano huo kwa niaba ya serikali zao katika hafla fupi iliyofanyika siku ya Jumanne. 
Ecuador inakuwa nchi ya pili baada ya Malta ambayo wiki iliyopita nayo ilianzisha uhusiano wa kidiplomasia na Tanzania katika ngazi ya mabalozi. Kama ilivyokuwa kwa Malta hati za makubaliano hayo zitawasilishwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. 
Wakizungumza mara baada ya kubadilisha hati , wawakilishi hao pamoja na kuonyesha kufurahishwa na uhusiano huo, pia walielezea namna gani wanavyoweza kukuza ushirikiano katika masuala mbalimbali yenye maslahi ya pande hizo mbili hapa Umoja wa Mataifa na nje ya Umoja wa Mataifa. 
“ Ni kwa muda mrefu serikali yangu ( Ecuador ) imekuwa ikitamani sana kuwa na uhusiano wa Tanzania, hatimaye leo ndoto na nia yetu imekamilika huu ni mwanzo mzuri, ninakushukuru sana Balozi Manongi na shukrani nyingi kwa serikali yako kwa kuridhia hatua hii muhimu” akasema Balozi Mendoza. 
Kwa upande wake, Balozi Tuvako Manongi amemwambia Balozi Mendoza kwamba, nchi hizo mbili zimefungua ukurasa mpya. 
Na akaongeza . “ ninatambua kwamba nchi yako ina mipango mizuri inayotekeleza katika uhifadhi wa maliasili hususani mbuga na misitu. Sisi tuna utajiri mkubwa wa misitu na mbunga nadhani tuna la kujifunza kutoka kwenu ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu. 
Ecuador iko katika eneo la Amerika ya Kusini, ambapo uchumi wake unaendeshwa pamoja na na sekta nyingine mafuta, kilimo na viwanda.
 Balozi   Tuvako   Manongi na  Balozi Xavier Mendoza,  wakisaini   kwa niaba ya serikali zao,  hati za kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia katika nganzi  ya Mabalozi katika hafla  fupi iliyofanyia siku ya  Jumanne, wanaoshuhudia ni  Maafisa  Waandamizi,  Bi.Tully Mwaipopo ( Tanzania) na  Bw. Agustin Fornell ( Ecuador)
 " Mambo sasa  safi kabisa" ndiyo wanavyosema  wawakilishi hawa wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako  Manongi wa Tanzania, na Xavier Mendoza wa Ecuador wakati wa kibadilisha  Hati za kuanzishwa kwa uhusiano kati ya  mataifa hayo mawili.
  " Uhusaino huu utatuwezesha  kujifunza na kubadilisha  uzoefu katika mambo mengi,  tena  nimegundua     mnamipango mizuri sana ya  kuhifadhi mazingira". Anasema Balozi Manongi
"kwa muda mrefu tumeisubiri siku hii,  asante sana na asante kwa serikali  yako kuridhia kuanzishwa kwa uhusiano huu, ni kweli   tunayomengi ya kujifunza  na kubadilisha uzoefu" anasema Balozi Mendoza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...