Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akikata utepe kuzindua mkutano  wa Kimataifa kuhusu Vitambulisho vya Taifa vya Kielektroniki, ulioanza leo jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Serena, Kulia kwa Naibu Waziri ni Waziri wa Maendeleo na Mshikamano wa  Jamii  wa Jamhuri ya Djibout, Zahar Youssuouf Kayad na Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) hapa nchini, Joseph Makani na kushoto ni Naibu Waziri wa Mawasiliano wa Ghana, Bw. Edward Ato Sarpong, na  Mwenyekiti wa Kampuni ya Asia Pacific Smart Card Association, Bw. Greg Pote.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima, akihutubia  katika mkutano wa Kimataifa wa Vitambulisho vya Taifa vya Kielektroniki Barani Afrika, ulioanza leo Jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Serena.  Mbele yake ni wageni toka mataifa mbalimbali  wanaohudhuria mkutano huo.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Maofisa wa moja ya makampuni yanayoshiriki katika mkutano wa Kimataifa wa Vitambulisho vya Taifa vya Kielektroniki Barani Afrika unaoendelea Jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Serena.
 Mmoja wa washiriki wa Maonyesho kuhusu Vitambulisho vya Kielektroniki yanayoendelea katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam, Cyrille Volentier  akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima kuhusu shughuli zinazofanywa na Kampuni yake inayojishughulisha na uchapishaji wa vitambulisho vya kielektroniki.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akipata maelezo kutoka kwa moja ya makampuni yanayoshiriki mkutano  wa Kimataifa wa  Vitambulisho vya Taifa vya Kielektroniki Barani Afrika unaoendelea Jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Serena.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...